Your choices on this site

We store a few things on your device so the radio works. Only if you agree, we also remember your settings and count how the site is used. We do not use advertising cookies today. “Marketing” is off unless you allow it: then a small script from the third-party service Metricool helps us understand visits from social media. You can change your mind at any time with Cookie settings at the bottom of every page. Cookie Policy

CatchliteRadio
Dakika 10 Za Kocha cover art

Dakika 10 Za Kocha

Karibu kwenye mafunzo ya Kocha Dr. Makirita Amani, MD, CFE. Mafunzo haya yamejengwa kwa kanuni ya MAARIFA + VITENDO = MAFANIKIO. Hapa unapata MAARIFA sahihi, ambayo ukiyaweka kwenye VITENDO utapata MAFANIKIO kwa uhakika. Maarifa haya yamejikita kwenye maeneo makuu matatu; MAFANIKIO ; Kujenga Tabia na Nidhamu sahihi kwa mafanikio. FEDHA ; Kujenga Utajiri na Uhuru wa Kifedha. BIASHARA ; Kujenga Biashara inayojiendesha bila kukutegemea. Karibu upate MAARIFA haya kwa kina kwa njia hizi; #BaruaZaKocha ; https://learn.tanzaniteskills.ac.tz/#/view/newsletter/4/13/ #Dakika10ZaKocha ; https://www.spreaker.com/podcast/dakika-10-za-kocha--1923276 #AmkaNaKocha ; https://amkamtanzania.com/ #OngeaNaKocha ; https://www.youtube.com/@onkocha #WashirikaWaMafanikio (Kundi); https://chat.whatsapp.com/DldGMa1wCi71SlPb4iuMKZ Karibu ujifunze na kubadili maisha yako. Kocha Dr. Makirita Amani, MD, CFE. Become a supporter of this podcast: https://www.spreaker.com/podcast/dakika-10-za-kocha--1923276/support .

A podcast cover with a progress bar showing where you stopped

Pick up right where you left off

  • Resume on any device
  • Progress saved on every episode
  • Plus every other Pro feature

From €2.49/month

Episodes

  • #DZK029; Njia Rahisi Ya Kubadili Tabia Ili Ufanikiwe.

    Jun 30, 2026 · 10m

    Resume with Pro

    Njia Rahisi Ya Kubadili Tabia Zako. Rafiki, Moja ya vitu vilivyosimama kati yako na mafanikio yako ni tabia ulizonazo. Huwa tunajenga tabia, halafu baadaye tabia zinatujenga sisi. Ili upate matokeo ya tofauti na unayopata sasa, lazima uwe na tabia tofauti na ulizonazo sasa. Lakini kubadili tabia siyo kitu rahisi. Umejaribu mara nyingi kujenga tabia mpya lakini unakwama. Hiyo ni kwa sababu...

  • #DZK028; Mantiki, Ushahidi Na Matumizi - Vigezo Sahihi Vya Mafanikio.

    Jun 29, 2026 · 10m

    Resume with Pro

    Tumia Mantiki, Ushahidi Na Matumizi Kuepuka Usumbufu Rafiki, Naweza kukupa sababu kubwa inayokukwamisha kufanikiwa. Sababu hiyo ni usumbufu. Kuhangaika na mambo mengi ambayo hayana tija kabisa. Unaweza kudhani mambo unayohangaika nayo sasa yana mchango kwako. Lakini siyo. Lipo chujio kali la kujua kipi kina mantiki na kipi hakina. Chujio hilo linaangalia vitu vitatu; 1. Mantiki - Ina maana gani...

  • #DZK027; Jitofautishe Hivi Na Akili Mnemba (AI)

    Jun 27, 2026 · 10m

    Resume with Pro

    Je AI Itakuacha Salama? Rafiki, Teknolojia nyingi zimekuja duniani, Ambazo zimefanya maisha yetu binadamu kuwa bora. Kila teknolojia imekuwa inategemea sana mwongozo wa binadamu ili ifanye kazi. Lakini sasa hivi tuko kwenye mapinduzi ya teknolojia ambayo ni ya tofauti kabisa. Teknolojia hii haitegemei sana mwongozo wa binadamu, bali inaweza kujiongoza yenyewe. Teknolojia hii siyo tena kifaa cha...

  • #DZK026; Epuka Huu Upumbavu Wa Kujitakia Unaokukwamisha Kufanikiwa.

    Jun 26, 2026 · 10m

    #BZK; Epuka Huu Upumbavu Wa Kujitakia Unaokukwamisha Kufanikiwa. Rafiki, Hatua muhimu sana kwenye safari ya mafanikio makubwa ni kuepuka kuwa mpumbavu. Hiyo ni kwa sababu upumbavu ni mzigo ambao ni vigumu sana mtu kuutua. Wakati ujinga inawezekana kuutua kwa kujifunza, upumbavu huwa unamganda mtu kwa muda mrefu. Huwa kuna aina mbili za upumbavu. Ya kwanza ni ule upumbavu wa msingi ambao mtu...

  • #DZK025; Usibadilike Kuendana Na Dunia, Ibadili Dunia Iendane Na Wewe.

    Jun 25, 2026 · 10m

    Ibadili Dunia, Iendane na Wewe. Rafiki, Watu wa kawaida huwa wanabadilika kuendana na dunia. Watu wasio wa kawaida huwa wanaibadili dunia kuendana nao. Je unadhani ni kundi lipi linaloleta mafanikio makubwa? Jibu ni kundi la wanaoibadili dunia. Sasa kama unajua hivyo, mbona bado unakazana kubadilika ili uendane na dunia? Kwenye #BaruaYaKocha nimekueleza kwa kina jinsi ya kuibadili dunia iendane...

  • #DZK024; Kufanikiwa, Ondoka Ukanda Wa Faraja Kwenda Ukanda Wa Ukuaji.

    Jun 24, 2026 · 10m

    Jenga Ushahidi Sahihi Wa Mafanikio. Rafiki, Mambo mengi tunayofanya ni kwa msukumo wa ushahidi tunaopata. Na kutokana na ushahidi huo, tuna kanda tatu tunazoweza kuwa kifikra. Moja ni ukanda wa faraja (comfort zone) ambapo tunapata ushahidi tuliozoea. Mbili ni ukanda wa ukuaji (growth zone) ambapo tunapata ushahidi chanya. Na tatu ni ukanda wa utisho (panic zone) ambapo tunapata ushahidi hasi...

  • #DZK023; Njia Rahisi Ya Kuwabadilisha Watu Wakubaliane Na Wewe.

    Jun 23, 2026 · 10m

    Wabadilishe watu bila kuwabadilisha. Rafiki, Najua kuna watu wengi sana unaotaka kuwabadilisha ili wawe vile unavyotaka wewe. Labda ni mwenza wako, ambaye ana tabia fulani usizozipenda. Wanaweza kuwa watoto, ambao unataka wajenge tabia sahihi za mafanikio. Au wafanyakazi ambao unataka wajitume zaidi kwenye majukumu yao. Ukijaribu kuwalazimisha watu wabadilike, ndiyo unakuwa umewaambia...

  • #DZK022; Soma, Andika na Fundisha Ili Ufanikiwe.

    Jun 22, 2026 · 10m

    Soma, Andika, Fundisha. Rafiki, Kuna kanuni rahisi sana ya mafanikio, Ambayo ukiifuata, utaweza kujenga ubobezi na ushawishi mkubwa. Kanuni hiyo ni ya *K Tatu; Kusoma, Kuandika na Kufundisha.* Unatakiwa *KUSOMA* ili kujifunza. *KUANDIKA* ili kuelewa. Na *KUFUNDISHA* ili kubobea. Kwenye #BaruaYaKocha nimekuonyesha jinsi unavyoweza kutumia hayo matatu kufanya makubwa na kufanikiwa. Isome barua hiyo...

  • #DZK021; Usijenge Msingi Wa Mafanikio Kwenye Mchanga.

    Jun 20, 2026 · 10m

    Acha Kujenga Msingi Wa Mafanikio Kwenye Mchanga Rafiki, Unapambana sana kufanikiwa. Lakini mafanikio yanakuwa magumu kufikia. Na hata ukiyapata, hayadumu. Hilo halisababishwi na mafanikio kushindikana. Bali linasababishwa na msingi unaojenga wa mafanikio. Wengi wanahangaika kujenga msingi wa mafanikio kwenye mchanga. Dhoruba kidogo inapotokea, inasambaratisha kila kitu. Kwenye #BaruaYaKocha...

  • #DZK020; Hamasa, Jasho Na Hatari Kwenye Safari Ya Mafanikio Makubwa.

    Jun 19, 2026 · 10m

    Hamasa, Jasho na Hatari Rafiki, Mafanikio makubwa yanaenda kwa kanuni hii; 1. Hamasa - 10% 2. Jasho (Kazi) - 90% 3. Hatari - Mara zote. Watu wengi wanakwama kufanikiwa kwa sababu wanageuza kanuni hiyo. Wanadhani hamasa pekee inawatosha kufanikiwa. Wanakwepa kuweka kazi kubwa inayohitajika. Na wanakwepa hatari. Kama unafanya chochote kati ya hivyo, jua unajikwamisha mwenyewe kufanikiwa. Kwenye...

  • #DZK019; Tumaini Unalohitaji Ili Kufanikiwa Kwa Uhakika

    Jun 18, 2026 · 10m

    Ukiwa na Tumaini Hili, Hakuna Kitakachokushinda. Rafiki, Pamoja na wengi kutaka mafanikio makubwa kwenye maisha yao, Ni wachache sana wanaoyapata. Na siyo kwa sababu mafanikio yamewekwa kwa ajili ya wachache. Bali ni kwa sababu wengi wanakosa Tumaini la kuendelea na safari, hasa mambo yanapokuwa magumu. Kwenye #BaruaYaKocha nimekushirikisha Tumaini ambalo ukilijenga, hakipo kinachoweza...

  • #DZK018; Okoa Muda Na Nguvu, Ufanikiwe.

    Jun 17, 2026 · 10m

    Unapoteza Rasilimali Muhimu Bila Tija. Rafiki, Muda wako na nguvu zako ni rasilimali muhimu sana kwako. Hizo ndiyo rasilimali kuu zinazohitajika kwenye kujenga mafanikio makubwa. Lakini pia ni rasilimali zenye uhaba mkubwa. Una ukomo wa muda na nguvu zako zinaisha kila unapozitumia. Cha kushangaza, licha ya ukomo wa rasilimali hizo, umekuwa unazipoteza bila tija. Umekuwa unafanya mambo...

  • #DZK017; Raha Rahisi Zinakupoteza

    Jun 16, 2026 · 10m

    RAHA RAHISI, MAFANIKIO MAGUMU. Rafiki, Moja ya vitu vinavyokuzuia kupata mafanikio makubwa ni raha unazopata kwa urahisi. Mambo mengi tunayofanya ni kwa ajili ya kupata raha. Na pale raha inapopatikana kirahisi, kama kupitia ulevi, mitandao na kufanya mapenzi, inazuia kufanya makubwa yanayohitajika kwenye mafanikio. Kwenye #BaruaYaKocha nimekuonyesha jinsi ya kukwepa mtego huo wa Raha Rahisi ili...

  • #DZK016; Jiamini Kupitiliza Upate Mafanikio Makubwa

    Jun 15, 2026 · 10m

    MAFANIKIO MAKUBWA HAYATOKANI NA AKILI ZA KAWAIDA. Soma hapa; https://learn.tanzaniteskills.... Rafiki, Umekuwa unayataka mafanikio makubwa, Lakini hujayapata mpaka sasa. Siyo kwa sababu haiwezekani, Bali kwa sababu njia unazotumia siyo sahihi. Njia kuu inayokupotosha ni wewe kutumia akili zako za kawaida. Hizo ndiyo akili zimekufikisha hapo ulipo sasa. Na kamwe, haziwezi kukufikisha zaidi ya hapo...

  • #DZK015; Fanikiwa Bila Kutegemea 'Koneksheni'

    Jun 13, 2026 · 10m

    Uhakika Wa Mafanikio Kama Unaanzia Chini. Soma hapa; https://learn.tanzaniteskills.... Rafiki yangu mpendwa, Unaanzia chini kabisa, Huna koneksheni, Huna akili nyingi, Huna urithi, Na huna fursa ambazo wengine wanazipata. Je kuna nafasi yoyote kwako kufanikiwa? Jibu ni NDIYO KUBWA. Mafanikio makubwa hayategemei sana unaanzia wapi, Bali yanategemea unaelekea wapi. Kwenye #BaruaYaKocha nimekueleza...

  • #DZK014; Unajinyima Pesa Wewe Mwenyewe.

    Jun 12, 2026 · 10m

    #BZK; KWA NINI UNAUPENDA SANA UMASIKINI? Soma hapa; https://learn.tanzaniteskills.... Rafiki, Huenda hilo swali limekushtua, Kwa sababu umekuwa unadhani kwamba unauchukia umasikini. Kwamba unapambana usiku na mchana ili uondoke kwenye umasikini. Lakini tunapoangalia mambo unayofanya, tunaona kabisa ni kinyume na hilo. Na hata matokeo unayopata sasa, yanaakisi kabisa hilo. Kwenye #BaruaYaKocha...

  • #BZK013; Jinsi ya Kujenga Biashara Kubwa Hata Kama Huna Mtaji.

    Jun 11, 2026 · 10m

    Biashara Bila Mtaji? Rafiki, Najua upo kwenye moja ya makundi haya mawili; Moja; Hujaanza biashara kwa sababu huna mtaji. Mbili; Una biashara ila haikui, kwa sababu huna mtaji. Ninachotaka kukuambia ni hiki; hakuna kundi sahihi hapo wewe kuwa. Unaweza kuanzisha na kukuza biashara kwa mafanikio makubwa, hata kama huna mtaji. Kwenye #BaruaYaKocha nimekuonyesha jinsi ya kufanya hivyo kwa uhakika...

  • #DZK012; Mfurahishe Mtu Huyu Mmoja Pekee Ili Ufanikiwe.

    Jun 10, 2026 · 10m

    Unajiangusha sana wewe mwenyewe. Rafiki, Kila unachofanya kwenye maisha yako, una bet kwenye furaha. Unadhani utakuwa na furaha zaidi kwa kufanya kitu hicho kuliko kutokukifanya. Mara nyingi, unashindwa kwenye kubet kwako, kwa sababu unaweka dau lako pasipo sahihi. Unaweka dau lako kwenye kutaka kuwafurahisha wengine. Wakati hilo ni jukumu usiloliweza kabisa. Una jukumu moja tu hapa duniani...

  • #DZK011; Usivurugwe Na Mapenzi Kwenye Safari Ya Mafanikio.

    Jun 9, 2026 · 10m

    Makosa Ya Kufanya Unachopenda. Rafiki, Ushauri wa mtu kufanya kile anachopenda ndiyo afanikiwe umewapoteza wengi sana. Kwenye mengi ambayo watu wanapenda kufanya, hayawezi kuwapa mafanikio wanayotaka. Swali ni je wewe unachukua hatua gani pale unachopenda kufanya hakiwezi kukupa mafanikio? Kwenye #BaruaYaKocha nimekuonyesha jinsi ya kutokuvurugwa na kufanya unachopenda kwenye safari ya mafanikio...

  • #DZK010; Vigezo Viwili Vya Kuamua Cha Kufanya Ili Ufanikiwe.

    Jun 8, 2026 · 10m

    Kama Unachofanya Kinakidhi Vigezo Hivi 2, Wapuuze Wanaokupinga. Rafiki, Safari ya mafanikio ina vikwazo na changamoto nyingi. Kuna miluzi mingi sana, ambapo kama hutakuwa makini, itakupoteza. Ili usipotezwe na hiyo miluzi mingi, kuna vigezo vikuu viwili unavyotakiwa kutumia kuchagua nini ufanye na nini upuuze. Kwenye #BaruaYaKocha nimeeleza kwa kina vigezo hivyo na jinsi ya kuvitumia. Isome barua...

  • #DZK009; Chagua Kwa Usahihi Kitakachokuua.

    Jun 6, 2026 · 10m

    KUBALI MAFANIKIO MAKUBWA YAKUUE. Rafiki, Kabla hujashtushwa na hilo, Nikukumbushe tu kwamba, *utakufa*. Na hutakufa tu hivi hivi, bali kuna kitu kitakachokuua. Swali ni je unachagua nini kikuue? Utakuwa tayari kukwepa kufanya kazi ngumu inayohitajika ili ufanikiwe, Halafu ufe kwa ulevi au ajali za kizembe? Unapoyakimbia mafanikio kwa sababu yana hatari, Unakuwa umezikubali hatari nyingine na...

  • #DZK008; Mafanikio Ni Kujua Hujui.

    Jun 5, 2026 · 10m

    MAFANIKIO NI KUJUA HUJUI. Rafiki, Unapoianza safari ya mafanikio, unakuwa hujui na hivyo unajifunza. Unapoanza kupata mafanikio, unaanza kuona tayari unajua na hivyo hujifunzi tena. Hapo ndipo unapokaribisha anguko la kimafanikio. Ili kupata na kudumu kwenye mafanikio makubwa, unapaswa kujua kitu kimoja; *JUA KWAMBA HUJUI* Kwa kujua hujui, unakuwa mnyenyekevu na kujifunza bila kukoma. Kwenye...

  • #DZK007; Usikubali Kushindwa Na Yeyote

    Jun 4, 2026 · 10m

    USIKUBALI KUSHINDWA NA YEYOTE. Rafiki, Ushindani ni sehemu ya safari yako ya mafanikio. Lolote utakalofanya na kuleta matokeo mazuri, watu watakuiga. Huwezi kuwashinda wengine kwa kushindana nao moja kwa moja. Badala yake kuna mbinu bora kabisa za kuwashinda wengine bila kusumbuka sana. Kwenye #BaruaYaKocha, nimekuonyesha mambo matano ya kukuwezesha kuwashinda wengine wote. Yajue mambo hayo kwa...

  • #DZK006; Pesa Inaweza Kununua Furaha.

    Jun 3, 2026 · 10m

    PESA INAWEZA KUNUNUA FURAHA Rafiki, Najua umeaminishwa kwamba utajiri hauwezi kukupa furaha. Na hiyo ndiyo sababu unakosa vyote, unakosa utajiri na pia unakosa furaha. Ili uweze kupata vyote, upate utajiri mkubwa na uwe na furaha, kuna mambo matano muhimu kuzingatia. Kwenye #BaruaYaKocha nimekushirikisha mambo hayo na jinsi ya kuyatumia kujenga utajiri na furaha. Soma barua hiyo hapa...

  • #DZK005; Baki Na Njaa Kali Ya Mafanikio Milele

    Jun 2, 2026 · 10m

    BAKI NA NJAA KALI YA MAFANIKIO. Rafiki, Unapokuwa unaanzia chini, unakuwa na njaa kali ya mafanikio. Njaa hiyo inakusukuma kufanya mambo makubwa na kupata matokeo makubwa. Lakini unapoanza kupata matokeo mazuri, hiyo njaa inaondoka. Na hapo ndipo anguko la wengi linapoanzia. Kama unataka kupata na kudumu kwenye mafanikio makubwa, unatakiwa kubaki na njaa kali ya mafanikio uliyoanza nayo. Kwenye...