Your choices on this site

We store a few things on your device so the radio works. Only if you agree, we also remember your settings and count how the site is used. We do not use advertising cookies today. “Marketing” is off unless you allow it: then a small script from the third-party service Metricool helps us understand visits from social media. You can change your mind at any time with Cookie settings at the bottom of every page. Cookie Policy

CatchliteRadio
Dakika 10 Za Kocha cover art

Dakika 10 Za Kocha

Karibu kwenye mafunzo ya Kocha Dr. Makirita Amani, MD, CFE. Mafunzo haya yamejengwa kwa kanuni ya MAARIFA + VITENDO = MAFANIKIO. Hapa unapata MAARIFA sahihi, ambayo ukiyaweka kwenye VITENDO utapata MAFANIKIO kwa uhakika. Maarifa haya yamejikita kwenye maeneo makuu matatu; MAFANIKIO ; Kujenga Tabia na Nidhamu sahihi kwa mafanikio. FEDHA ; Kujenga Utajiri na Uhuru wa Kifedha. BIASHARA ; Kujenga Biashara inayojiendesha bila kukutegemea. Karibu upate MAARIFA haya kwa kina kwa njia hizi; #BaruaZaKocha ; https://learn.tanzaniteskills.ac.tz/#/view/newsletter/4/13/ #Dakika10ZaKocha ; https://www.spreaker.com/podcast/dakika-10-za-kocha--1923276 #AmkaNaKocha ; https://amkamtanzania.com/ #OngeaNaKocha ; https://www.youtube.com/@onkocha #WashirikaWaMafanikio (Kundi); https://chat.whatsapp.com/DldGMa1wCi71SlPb4iuMKZ Karibu ujifunze na kubadili maisha yako. Kocha Dr. Makirita Amani, MD, CFE. Become a supporter of this podcast: https://www.spreaker.com/podcast/dakika-10-za-kocha--1923276/support .

A podcast cover with a progress bar showing where you stopped

Pick up right where you left off

  • Resume on any device
  • Progress saved on every episode
  • Plus every other Pro feature

From €2.49/month

Episodes

  • #DZK054; Uvumilivu Usio Na Subira Unaohitajika Kwenye Mafanikio Makubwa

    Jul 29, 2026 · 10m

    Resume with Pro

    Mafanikio Yanataka Uwe Na *'Uvumilivu Usio Na Subira.' Soma hapa; https://learn.tanzaniteskills.... Rafiki, Bill Gates amewahi kusema; *'Tunakadiria kwa ukubwa tunachoweza kufanya ndani ya mwaka mmoja na kukadiria kwa udogo tunachoweza kufanya ndani ya miaka 10.'* Hiyo ni kauli yenye nguvu sana na inayoonyesha kwa nini watu wengi wanashindwa. Unakuwa mtu usiye na uvumilivu, kwa kutaka mambo...

  • #DZK053; Mshinde Adui Huyu Anayekuhujumu Usifanikiwe.

    Jul 28, 2026 · 10m

    Resume with Pro

    Mshinde Adui Huyu Mmoja Na Mafanikio Yanakuwa Uhakika Kwako. Soma hapa; https://learn.tanzaniteskills.... Rafiki, Kila tamthilia huwa inakuwa na adui mkuu mmoja ambaye anakuwa vigumu sana kushindwa. Mhusika mkuu ni lazima apambane sana ndiyo aweze kumshinda adui huyo. Hivyo pia ndivyo maisha na mafanikio yako yalivyo. Kuna adui mkuu mmoja ambaye anakukwamisha sana. Usipomjua na kumshinda adui...

  • #DZK052; Turudi Kwenye Ujenzi Ili Tujenge Mafanikio Makubwa Na Ya Kudumu.

    Jul 27, 2026 · 10m

    Resume with Pro

    Acha Kufanya, Anza Kujenga. Soma hapa; https://learn.tanzaniteskills.... Rafiki, Unaweka juhudi kubwa sana kila siku, Unafanya kwa muda mrefu, Unapata matokeo ya muda mfupi, Lakini hupati mafanikio makubwa unayoyataka. Siyo bahati mbaya, Na siyo kwamba mafanikio hayawezekani kwako. Bali unachohangaika nacho ndiyo hakiwezi kukupa mafanikio unayotaka. Unahangaika na kufanya, badala ya kujenga...

  • #DZK051; Kuwa Mkamilifu Ujenge Mafanikio Yanayodumu.

    Jul 25, 2026 · 10m

    Jenga Huu Ukamilifu Ufanikiwe. Soma hapa; https://learn.tanzaniteskills.... Rafiki, Kupata na kudumu kwenye mafanikio makubwa inataka mtu uwe mkamilifu sana. Na sisi binadamu siyo wakamilifu. Tuna madhaifu mengi yanayotukwamisha kufanikiwa. Lakini kuna habari njema, Kuna ukamilifu ambao upo ndani ya uwezo wako kujijengea. Ukiwa na ukamilifu huo, kupata na kudumu kwenye mafanikio makubwa inakuwa...

  • #DZK050; Ushauri Sahihi Na Unaofanya Kazi Mara Zote.

    Jul 24, 2026 · 10m

    Epuka Huu Ushauri Unaokupotosha. Soma hapa; https://learn.tanzaniteskills.... Rafiki, Umekuwa unahangaika na ushauri mwingi, Ambao unakinzana wenyewe. Upande mmoja unashauriwa hivi, Upande mwingine unashauriwa kinyume na hivyo. Unajikuta njia panda na usijue cha kufanya. Kwenye #BaruaYaKocha nimekushirikisha ushauri sahihi na wa msingi kwenye maeneo muhimu kama fedha, kazi, muda na afya. Soma...

  • #DZK049; Pandisha Kodi Ya Pango Kwenye Akili Yako Ufanikiwe.

    Jul 23, 2026 · 10m

    Acha Kuifanya Akili Yako Kuwa Jalala. Soma hapa; https://learn.tanzaniteskills.... Rafiki, Akili yako ni mgodi wa dhahabu. Ina uwezo wa kukupa makubwa sana unayoyataka. Lakini umegeuza mgodi huo kuwa jalala, Kwa kuruhusu kila kitu kiingie. Matokeo yake ni unachoka, Huku ukishindwa kupiga hatua unazotaka. Kwenye #BaruaYaKocha nimekueleza jinsi ya kupandisha kodi ya pango kwenye akili yako, ili...

  • #DZK048; Mafanikio Yako Yanaamuliwa Na Madhaifu Na Siyo Uimara.

    Jul 22, 2026 · 10m

    Madhaifu Yanakukwamisha Sana. Soma hapa; https://learn.tanzaniteskills.... Rafiki, Umekuwa unapambana sana, Lakini bado unakwama. Siyo kwa sababu huwezi kufanikiwa, Bali kwa sababu hujajua nguvu ya madhaifu yako kwenye kukukwamisha. Kwenye #BaruaYaKocha nimekuonyesha jinsi unavyopaswa kuyazuia madhaifu yasiwe kikwazo. Isome barua hapa; https://learn.tanzaniteskills.... Madhaifu yana nguvu kubwa...

  • #DZK047; Kwa Nini Unaendelea Kuyang'ang'ania Maisha Mpaka Sasa?

    Jul 21, 2026 · 10m

    Kwa Nini Hujachukua Njia Ya Mkato Kumaliza Shida Zako? Soma hapa; https://learn.tanzaniteskills.... Rafiki, Kwenye maisha yako umepitia shida na changamoto mbalimbali. Nyingine zimekufikisha mpaka kwenye hali ya kukata tamaa. Na kuona hakuna namna ya kutoka kwenye hali hizo. Lakini pamoja na hayo yote, hujachukua njia ya mkato, ya kukatisha maisha yako ili kumaliza shida zako. Kwa maneno mengine...

  • #DZK046; Rasilimali Za Msingi Unazo Za Kutosha, Zitumie Vizuri Ufanikiwe.

    Jul 20, 2026 · 10m

    Tatizo Unachezea Matirio. Soma hapa; https://learn.tanzaniteskills.... Rafiki, Najua unasema hujafanikiwa kwa sababu unakosa rasilimali unazotaka. Unadhani ungepata muda zaidi ungefanya mengi. Unadhani ungepata fedha zaidi ungefanya kwa ukubwa zaidi. Vipi kama nikikuambia muda unao mwingi mpaka unaupoteza? Vipi kama nikikuonyesha fedha ulizonazo sasa, hata kama ni kidogo zinatosha kufanya makubwa...

  • #DZK045; Usiwabishie Watu Wanapokuonyesha Ukweli Wao.

    Jul 18, 2026 · 10m

    Watu Hawakudanganyi, Unajidanganya Mwenyewe. Soma hapa; https://learn.tanzaniteskills.... Rafiki, Najua umekuwa unalalamika pale watu wanapokudanganya. Wanakuambia vitu ambavyo unawaamini, Lakini kwenye utendaji, wanakuwa tofauti na walivyosema. Ni rahisi watu kudanganya kwa maneno, Lakini siyo kwa vitendo. Matendo ya watu hudhihirisha ukweli wao wote. Ni sisi tu kuwa makini kuyaangalia matendo...

  • #DZK044; 'Dogosha' Malengo Yako Uyafikie Kwa Uhakika.

    Jul 17, 2026 · 10m

    Dogosha Malengo Yako Uyafikie. Soma hapa; https://learn.tanzaniteskills.... Rafiki, Najua una malengo na mipango mikubwa sana. Na umekuwa unakazana sana kuifikia. Lakini nikuulize swali, Unawezaje kumla ng'ombe? Ni uhakika huwezi kumla mzima mzima. Bali utamkata vipande vidogo vidogo na kula. Hivyo pia ndivyo unavyopaswa kuyaendea malengo yako makubwa. Cha kushangaza, wewe umekuwa unapambana nayo...

  • #DZK043; Hakuna Kushindwa, Futa Neno Hilo Ufanikiwe.

    Jul 16, 2026 · 10m

    Kushindwa Ni Uongo. Soma hapa; https://learn.tanzaniteskills.... Rafiki, Kuna uongo mmoja ambao jamii imekuaminisha na wewe umeamini. Kuhusu kushindwa, Jamii imekuhubiria kuhusu kushindwa, Na wewe umeamini kuna mambo umeshindwa. Lakini ukweli ni huu, Hakuna kushindwa, Kushindwa ni kitu ambacho hakipo kabisa. Huenda ninachosema hapa nakuchanganya, Au unadhani nasema mambo ya kusadikika. Kwenye...

  • #DZK042; Hakuna Kinachosababisha Umasikini.

    Jul 15, 2026 · 10m

    Hakuna Kinachosababisha Umasikini. Soma hapa; https://learn.tanzaniteskills.... Rafiki, Kama umekuwa unajiuliza nini kinachosababisha umasikini, Jibu ni hakuna. Hakipo kinachosababisha umasikini. Na kama umekuwa unakitafuta, unapoteza muda wako bure. Muda wako utakuwa na thamani kubwa kama utautumia kujua kinachosababisha utajiri na kufanyia kazi. Kwenye #BaruaYaKocha unakwenda kujifunza kwa nini...

  • #DZK041; Kanuni Ya Kujijengea Nidhamu Kali Ya Mafanikio.

    Jul 14, 2026 · 10m

    Kanuni Ya Kujenga Nidhamu Kali Itakayokupa Mafanikio Makubwa. Soma hapa; https://learn.tanzaniteskills.... Rafiki, Tunajua umuhimu wa nidhamu kali kwenye kujenga mafanikio makubwa. Lazima upange na kutekeleza ndiyo upate mafanikio. Lakini wengi wanakwama, kwa sababu wanachukulia nidhamu kama kujitesa. Ukweli ni kwamba, nidhamu siyo mateso. Ipo kanuni ya nidhamu ambayo haina kabisa mateso. Kanuni...

  • #DZK040; Uko 'Siriazi' Na Mafanikio Makubwa Kweli?

    Jul 13, 2026 · 10m

    Hivi Uko 'Serious' Kweli? Soma hapa; https://learn.tanzaniteskills.... Rafiki, Umejisikiaje baada ya kusikia hilo swali? Mtu anapokuuliza kama upo serious juu ya jambo fulani, lazima ujitafajari. Na mimi nataka tu kukuambia, Unasema sana kwamba unayataka mafanikio. Lakini kuna tatizo moja, Hujawa serious kweli kweli kuyapata. Ndiyo, namaanisha hilo na ushahidi ninao. Kwenye #BaruaYaKocha...

  • #DZK039; Poteza Matokeo, Lakini Usipoteze Tabia.

    Jul 11, 2026 · 10m

    Poteza Matokeo, Lakini Usipoteze Tabia. Soma hapa; https://learn.tanzaniteskills.... Rafiki, Safari ya mafanikio ni ligi inayochezwa kwa kipindi chote cha maisha yako. Kwenye ligi yoyote, mafanikio siyo kushinda michezo yote. Kuna michezo ambayo utapoteza. Lakini kama utabaki na tabia na mchakato wako, bado utafanikiwa. Kinachowazuia wengi kufanikiwa ni pale wanaporuhusu matokeo mabaya kubadili...

  • #DZK038; Geuza Udhaifu Wako Kuwa Uimara Wa Mafanikio.

    Jul 10, 2026 · 10m

    Geuza Udhaifu Wako Kuwa Uimara Wa Mafanikio. Soma hapa; https://learn.tanzaniteskills.... Rafiki, Sisi binadamu hatujakamilika. Huwa tuna madhaifu mengi ambayo huwa ni kikwazo kwa mafanikio tunayoyataka. Elimu, mafunzo na ushauri mwingi tunaopata huwa unatutaka tuboreshe madhaifu yetu. Matokeo ya hilo ni tunajikuta tukiwa na madhaifu imara zaidi, na hivyo kujikwamisha zaidi. Kwenye #BaruaYaKocha...

  • #DZK037; Jiamulie Mambo Ili Ufanikiwe.

    Jul 9, 2026 · 10m

    Jiamulie Mambo Ili Ufanikiwe. Soma hapa; https://learn.tanzaniteskills.... Rafiki, Unajikwamisha kupata mafanikio makubwa, Kwa sababu ya kusubiri watu wakuamulie au wakuruhusu ufanye unachotaka. Haijawahi kutokea kwa yeyote aliyepata mafanikio makubwa, Kusubiri aruhusiwe na mtu yeyote yule. Mafanikio makubwa yanataka *uwe mtu wa kujiamulia mambo.* Kwenye #BaruaYaKocha nimekuonyesha jinsi ya...

  • #DZK036; Akili Tatu Za Kujenga Mafanikio Makubwa.

    Jul 8, 2026 · 10m

    Akili Moja Haikutoshi Kufanikiwa. Soma hapa; https://learn.tanzaniteskills.... Rafiki, Unakazana sana kufanikiwa lakini unakwama. Kwa sababu unatumia akili yako moja tu, ambayo inafikiri. Lakini una akili tatu, moja ni hiyo uliyozoea kutumia. Na nyingine mbili zipo, ambazo zina nguvu kubwa sana. Kwenye #BaruaYaKocha nimekueleza kuhusu akili tatu ulizonazo na jinsi ya kuzitumia zote kufanikiwa...

  • #DZK035; Ushauri Wa Miaka 218 Unaokufaa Zaidi Leo.

    Jul 7, 2026 · 10m

    Hakuna Kipya Chini Ya Jua. Rafiki, Umekuwa unakazana kutafuta siri za mafanikio kama vile ni kitu kipya. Ambacho unasahau ni kwamba, hakuna kitu kipya kwenye hii dunia. Yote tunayoyaona yamekuwepo miaka kwa miaka. Napoleon, aliyekuwa mtawala wa Ufaransa aliandika barua kwa ndugu yake, aliyekuwa mtawala wa ufalme mwingine. Barua hiyo aliiandika mwaka 1808 na ilieleza vitu vitatu vya mtu kufanya...

  • #DZK034; Epuka Fedha Kuwa Kikwazo Kwako Kufanikiwa.

    Jul 6, 2026 · 10m

    Tamaa Ya Pesa Inakuzuia Kupata Pesa Zaidi. Rafiki, Kama unasoma hapa, Najua unataka kupata pesa zaidi. Lakini kupata pesa inapokuwa ndiyo kipaumbele pekee kwako, Unakuwa unajizuia kupata pesa nyingi zaidi. Na hiyo siyo kwa sababu ya udhaifu wako, Bali ni kwa asili ya binadamu, Ipo kanuni inayosema; *Kipimo kinapogeuka lengo, kinaacha kuwa kipimo kizuri.* Hivyo ndivyo pesa inavyokuwa kikwazo...

  • #DZK033; Epuka Huu Utani Unaokukwamisha Kufanikiwa.

    Jul 4, 2026 · 10m

    Kataa Kabisa Huu Utani Kwenye Maisha Yako. Rafiki, Kuna vitu huwa tunavichukulia kama utani, Lakini vinakuwa na madhara makubwa kwenye maisha yetu. Moja ya vitu hivyo ni fikra na kauli hasi. Unapojiambia vitu hasi, hata kama ni kwa utani, vinakuathiri. Kwenye #BaruaYaKocha nimekuonyesha jinsi chochote hasi kinavyoweza kukukwamisha. Nimekuonyesha jinsi unavyopaswa kuwa mkali kuondoa kila kilicho...

  • #DZK032; Kuwa Mvumilivu Kwenye Kutokuwa Na Uhakika Ufanikiwe.

    Jul 3, 2026 · 10m

    Kuwa na Uvumilivu Kwenye Kutokuwa na Uhakika. Rafiki, Sisi binadamu huwa tunapenda sana uhakika. Hiyo ndiyo kazi namba moja ya ubongo wetu. Ndiyo maana tunaweza kubaki kwenye mambo yasiyotupa matokeo makubwa, kwa sababu tu yana uhakika. Ili tupate mafanikio makubwa, lazima tuweze kuvumilia hali ya kutokuwa na uhakika. Kwenye #BaruaYaKocha nimekupa mwongozo wa kujenga tabia hiyo. Soma barua hiyo...

  • #DZK031; Jipe Laana Ya Ushindi Ufanikiwe Kwa Uhakika

    Jul 2, 2026 · 10m

    Jipe Laana Ya Ushindi Ili Ufanikiwe. Rafiki, Kuna mambo unayorudia rudia kufanya na yanakukwamisha kupata mafanikio makubwa unayoyataka. Huenda unaamini mambo hayo ndiyo hatima yako. Au umelaaniwa usipate mafanikio unayoyataka. Nina habari njema sana kwako rafiki yangu, Kwamba, unaweza kujipa laana ya ushindi. Ndiyo, unaweza kujipa laana ambayo hata iweje, ni lazima utapata ushindi. Kwa laana...

  • #DZK030; Jinsi Ya Kupenda Chochote Ili Ufanikiwe.

    Jul 1, 2026 · 10m

    Kitendawili Cha Mapenzi Na Mafanikio. Rafiki, Kuna kitendawili cha muda mrefu kuhusu mapenzi na mafanikio. Watu wengi wameshindwa kutengua kitendawili hicho na hilo linawakwamisha. Mapenzi na Mafanikio ni vitu ambavyo haviwezi kutenganishwa. Ni lazima mtu apende sana kile anachofanya ndiyo aweze kupata mafanikio. Wengi wanahangaika na vitu wanavyopenda, wakati haviwezi kuwapa mafanikio. Ambacho...